4. BWANA yu katika hekalu lake takatifu.BWANA ambaye kiti chake kiko mbinguni,Macho yake yanaangalia;Kope zake zinawajaribu wanadamu.
5. BWANA humjaribu mwenye haki;Bali nafsi yake humchukia asiye haki,Na mwenye kupenda udhalimu.
6. Awanyeshee wasio haki mitego,Moto na kiberiti na upepo wa hari,Na viwe fungu la kikombe chao.