1. Ee Mungu wa sifa zangu, usinyamaze,
2. Kwa maana wamenifumbulia kinywa;Kinywa cha mtu asiye haki, cha hila,Wamesema nami kwa ulimi wa uongo.
3. Naam, kwa maneno ya chuki wamenizunguka,Wamepigana nami bure.
4. Badala ya upendo wangu wao hunishitaki,Ijapokuwa naliwaombea.
5. Wamenichukuza mabaya badala ya mema,Na chuki badala ya upendo wangu.
6. Uweke mtu mkorofi juu yake,Mshitaki asimame mkono wake wa kuume.
7. Katika kuhukumiwa ataonekana hana haki,Na sala yake itadhaniwa kuwa ni dhambi.
8. Siku zake na ziwe chache,Usimamizi wake na atwae mtu mwingine.
9. Wanawe na wawe yatima,Na mkewe na awe mjane.
10. Kutanga na watange wanawe na kuomba,Watafute chakula mbali na mahame yao.