Zab. 108:7-10 Swahili Union Version (SUV)

7. Mungu amenena kwa utakatifu wake,Nami nitashangilia.Nitaigawanya Shekemu,Nitalipima bonde la Sukothi.

8. Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu,Na Efraimu ni nguvu ya kichwa changu.Yuda ni fimbo yangu ya kifalme,

9. Moabu ni bakuli langu la kunawia.Nitamtupia Edomu kiatu changu,Na kumpigia Filisti kelele za vita.

10. Ni nani atakayenipeleka hata mji wenye boma?Ni nani atakayeniongoza hata Edomu?

Zab. 108