3. Ee BWANA, nitakushukuru kati ya watu,Nitakuimbia zaburi kati ya mataifa.
4. Maana fadhili zako ni kubwa hata mbinguni,Na uaminifu wako hata mawinguni.
5. Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.
6. Ili wapenzi wako waopolewe,Uokoe kwa mkono wako wa kuume, uniitikie.
7. Mungu amenena kwa utakatifu wake,Nami nitashangilia.Nitaigawanya Shekemu,Nitalipima bonde la Sukothi.