Zab. 107:40-42 Swahili Union Version (SUV)

40. Akawamwagia wakuu dharau,Na kuwazungusha katika nyika isiyo na njia.

41. Akamweka mhitaji juu mbali na mateso,Akamfanyia jamaa kama kundi la kondoo.

42. Wanyofu wa moyo wataona na kufurahi,Na uovu wa kila namna utajifumba kinywa.

Zab. 107