15. Na wamshukuru BWANA kwa fadhili zake,Na maajabu yake kwa wanadamu.
16. Maana ameivunja milango ya shaba,Ameyakata mapingo ya chuma.
17. Wapumbavu, kwa sababu ya ukosaji wao,Na kwa sababu ya maovu yao, hujitesa.
18. Nafsi zao zachukia kila namna ya chakula,Wameyakaribia malango ya mauti.
19. Wakamlilia BWANA katika dhiki zao,Akawaponya na shida zao.
20. Hulituma neno lake, huwaponya,Huwatoa katika maangamizo yao.
21. Na wamshukuru BWANA kwa fadhili zake,Na maajabu yake kwa wanadamu.
22. Na wamtolee dhabihu za kushukuru,Na kuyasimulia matendo yake kwa kuimba.
23. Washukao baharini katika merikebu,Wafanyao kazi yao katika maji mengi,
24. Hao huziona kazi za BWANA,Na maajabu yake vilindini.
25. Maana husema, akavumisha upepo wa dhoruba,Ukayainua juu mawimbi yake.
26. Wapanda mbinguni, watelemka vilindini,Nafsi yao yayeyuka kwa hali mbaya.
27. Wayumba-yumba, wapepesuka kama mlevi,Akili zao zote zawapotea.
28. Wakamlilia BWANA katika dhiki zao,Akawaponya na shida zao.
29. Huituliza dhoruba, ikawa shwari,Mawimbi yake yakanyamaza.