Zab. 107:10-21 Swahili Union Version (SUV)

10. Waliokaa katika giza na uvuli wa mauti,Wamefungwa katika taabu na chuma,

11. Kwa sababu waliyaasi maneno ya Mungu,Wakalidharau shauri lake Aliye juu.

12. Hata akawadhili moyo kwa taabu,Wakajikwaa wala hakuna msaidizi.

13. Wakamlilia BWANA katika dhiki zao,Akawaponya na shida zao.

14. Aliwatoa katika giza na uvuli wa mauti,Akayavunja mafungo yao.

15. Na wamshukuru BWANA kwa fadhili zake,Na maajabu yake kwa wanadamu.

16. Maana ameivunja milango ya shaba,Ameyakata mapingo ya chuma.

17. Wapumbavu, kwa sababu ya ukosaji wao,Na kwa sababu ya maovu yao, hujitesa.

18. Nafsi zao zachukia kila namna ya chakula,Wameyakaribia malango ya mauti.

19. Wakamlilia BWANA katika dhiki zao,Akawaponya na shida zao.

20. Hulituma neno lake, huwaponya,Huwatoa katika maangamizo yao.

21. Na wamshukuru BWANA kwa fadhili zake,Na maajabu yake kwa wanadamu.

Zab. 107