1. Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema,Kwa maana fadhili zake ni za milele.
2. Na waseme hivi waliokombolewa na BWANA,Wale aliowakomboa na mkono wa mtesi.
3. Akawakusanya kutoka nchi zote,Mashariki na magharibi, kaskazini na kusini.
4. Walitanga-tanga jangwani katika njia ya nyika;Hawakuona mji wa kukaa.
5. Waliona njaa, waliona na kiu,Nafsi yao ilikuwa ikizimia ndani yao.
6. Wakamlilia BWANA katika dhiki zao,Akawaponya na shida zao.
7. Akawaongoza kwa njia ya kunyoka,Wapate kwenda mpaka mji wa kukaa.
8. Na wamshukuru BWANA, kwa fadhili zake,Na maajabu yake kwa wanadamu.
9. Maana hushibisha nafsi yenye shauku,Na nafsi yenye njaa huijaza mema.
10. Waliokaa katika giza na uvuli wa mauti,Wamefungwa katika taabu na chuma,
11. Kwa sababu waliyaasi maneno ya Mungu,Wakalidharau shauri lake Aliye juu.
12. Hata akawadhili moyo kwa taabu,Wakajikwaa wala hakuna msaidizi.