Zab. 106:35-47 Swahili Union Version (SUV)

35. Bali walijichanganya na mataifa,Wakajifunza matendo yao.

36. Wakazitumikia sanamu zao,Nazo zikawa mtego kwao.

37. Naam, walitoa wana wao na binti zaoKuwa dhabihu kwa mashetani.

38. Wakamwaga damu isiyo na hatia,Damu ya wana wao na binti zao,Waliowatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani;Nchi ikatiwa unajisi kwa damu.

39. Ndivyo walivyotiwa uchafu kwa kazi zao,Wakafanya uasherati kwa matendo yao.

40. Hasira ya BWANA ikawaka juu ya watu wake,Akauchukia urithi wake.

41. Akawatia mikononi mwa mataifa,Nao waliowachukia wakawatawala.

42. Adui zao wakawaonea,Wakatiishwa chini ya mkono wao.

43. Mara nyingi aliwaponya,Bali walikuwa wakimwasi kwa mashauri yao,Wakadhilika katika uovu wao.

44. Lakini aliyaangalia mateso yao,Aliposikia kilio chao.

45. Akawakumbukia agano lake;Akawahurumia kwa wingi wa fadhili zake;

46. Akawajalia kuhurumiwaNa watu wote waliowateka.

47. Ee BWANA, Mungu wetu, utuokoe,Utukusanye kwa kututoa katika mataifa,Tulishukuru jina lako takatifu,Tuzifanyie shangwe sifa zako.

Zab. 106