26. Ndipo alipowainulia mkono wake,Ya kuwa atawaangamiza jangwani,
27. Na kuwatawanya wazao wao kati ya mataifa,Na kuwatapanya katika nchi mbali.
28. Wakajiambatiza na Baal-Peori,Wakazila dhabihu za wafu.
29. Wakamkasirisha kwa matendo yao;Tauni ikawashambulia.
30. Ndipo Finehasi akasimama akafanya hukumu;Tauni ikazuiliwa.
31. Akahesabiwa kuwa ana hakiKizazi baada ya kizazi hata milele.
32. Wakamghadhibisha penye maji ya Meriba,Hasara ikampata Musa kwa ajili yao,
33. Kwa sababu waliiasi roho yake,Akasema yasiyofaa kwa midomo yake.
34. Hawakuwaharibu watu wa nchiKama BWANA alivyowaambia;
35. Bali walijichanganya na mataifa,Wakajifunza matendo yao.
36. Wakazitumikia sanamu zao,Nazo zikawa mtego kwao.