Zab. 106:23-33 Swahili Union Version (SUV)

23. Akasema ya kuwa atawaangamizaKama Musa, mteule wake, asingalisimama,Mbele zake kama mahali palipobomoka,Ili aigeuze hasira yake asije akawaharibu.

24. Wakaidharau nchi ile ya kupendeza,Wala hawakuliamini neno lake.

25. Bali wakanung’unika hemani mwao,Wala hawakuisikiliza sauti ya BWANA.

26. Ndipo alipowainulia mkono wake,Ya kuwa atawaangamiza jangwani,

27. Na kuwatawanya wazao wao kati ya mataifa,Na kuwatapanya katika nchi mbali.

28. Wakajiambatiza na Baal-Peori,Wakazila dhabihu za wafu.

29. Wakamkasirisha kwa matendo yao;Tauni ikawashambulia.

30. Ndipo Finehasi akasimama akafanya hukumu;Tauni ikazuiliwa.

31. Akahesabiwa kuwa ana hakiKizazi baada ya kizazi hata milele.

32. Wakamghadhibisha penye maji ya Meriba,Hasara ikampata Musa kwa ajili yao,

33. Kwa sababu waliiasi roho yake,Akasema yasiyofaa kwa midomo yake.

Zab. 106