Zab. 105:32-44 Swahili Union Version (SUV)

32. Badala ya mvua aliwapa mvua ya mawe,Na moto wa miali katika nchi yao.

33. Akaipiga mizabibu yao na mitini yao,Akaivunja miti ya mipaka yao.

34. Alisema, kukaja nzige,Na tunutu wasiohesabika;

35. Wakaila miche yote ya nchi yao,Wakayala matunda ya ardhi yao.

36. Akawapiga wazaliwa wa kwanza katika nchi,Malimbuko ya nguvu zao.

37. Akawatoa hali wana fedha na dhahabu,Katika kabila zao asiwepo mwenye kukwaa.

38. Misri ilifurahi walipoondoka,Maana kwa ajili yao hofu imewaangukia.

39. Alitandaza wingu liwe funiko,Na moto utoe nuru usiku.

40. Walipotaka akaleta kware,Akawashibisha chakula cha mbinguni.

41. Akaufunua mwamba, kukabubujika maji,Yakapita pakavuni kama mto.

42. Maana alilikumbuka neno lake takatifu,Na Ibrahimu, mtumishi wake.

43. Akawatoa watu wake kwa shangwe,Na wateule wake kwa nyimbo za furaha.

44. Akawapa nchi za mataifa, wakairithi kazi ya watu;

Zab. 105