Zab. 105:21-32 Swahili Union Version (SUV)

21. Akamweka kuwa bwana wa nyumba yake,Na mwenye amri juu ya mali zake zote.

22. Awafunge masheki wake kama apendavyo,Na kuwafundisha wazee wake hekima.

23. Israeli naye akaingia Misri,Yakobo akawa mgeni katika nchi ya Hamu.

24. Akawajalia watu wake wazae sana,Akawafanya kuwa hodari kuliko watesi wao.

25. Akawageuza moyo wawachukie watu wake,Wakawatendea hila watumishi wake.

26. Akamtuma Musa, mtumishi wake,Na Haruni ambaye amemchagua.

27. Akaweka mambo ya ishara zake kati yao,Na miujiza katika nchi ya Hamu.

28. Alituma giza, kukafunga giza,Wala hawakuyaasi maneno yake.

29. Aliyageuza maji yao yakawa damu,Akawafisha samaki wao.

30. Nchi yao ilijaa vyura,Vyumbani mwa wafalme wao.

31. Alisema, kukaja makundi ya mainzi,Na chawa mipakani mwao mwote.

32. Badala ya mvua aliwapa mvua ya mawe,Na moto wa miali katika nchi yao.

Zab. 105