8. Yakapanda milima, yakatelemka mabondeni,Mpaka mahali ulipoyatengenezea.
9. Umeweka mpaka yasiupite,Wala yasirudi kuifunikiza nchi.
10. Hupeleka chemchemi katika mabonde;Zapita kati ya milima;
11. Zamnywesha kila mnyama wa kondeni;Punda mwitu huzima kiu yao.
12. Kandokando hukaa ndege wa angani;Kati ya matawi hutoa sauti zao.
13. Huinywesha milima toka orofa zake;Nchi imeshiba mazao ya kazi zako.
14. Huyameesha majani kwa makundi,Na maboga kwa matumizi ya mwanadamu;Ili atoe chakula katika nchi,
15. Na divai imfurahishe mtu moyo wake.Aung’aze uso wake kwa mafuta,Na mkate umburudishe mtu moyo wake.
16. Miti ya BWANA nayo imeshiba,Mierezi ya Lebanoni aliyoipanda.
17. Ndimo ndege wafanyamo vitundu vyao,Na korongo, misunobari ni nyumba yake.