8. Yakapanda milima, yakatelemka mabondeni,Mpaka mahali ulipoyatengenezea.
9. Umeweka mpaka yasiupite,Wala yasirudi kuifunikiza nchi.
10. Hupeleka chemchemi katika mabonde;Zapita kati ya milima;
11. Zamnywesha kila mnyama wa kondeni;Punda mwitu huzima kiu yao.
12. Kandokando hukaa ndege wa angani;Kati ya matawi hutoa sauti zao.
13. Huinywesha milima toka orofa zake;Nchi imeshiba mazao ya kazi zako.
14. Huyameesha majani kwa makundi,Na maboga kwa matumizi ya mwanadamu;Ili atoe chakula katika nchi,
15. Na divai imfurahishe mtu moyo wake.Aung’aze uso wake kwa mafuta,Na mkate umburudishe mtu moyo wake.