26. Ndimo zipitamo merikebu,Ndimo alimo lewiathani uliyemwumba acheze humo.
27. Hao wote wanakungoja Wewe,Uwape chakula chao kwa wakati wake.
28. Wewe huwapa,Wao wanakiokota;Wewe waukunjua mkono wako,Wao wanashiba mema;
29. Wewe wauficha uso wako,Wao wanafadhaika;Waiondoa pumzi yao, wanakufa,Na kuyarudia mavumbi yao,
30. Waipeleka roho yako, wanaumbwa,Nawe waufanya upya uso wa nchi.
31. Utukufu wa BWANA na udumu milele;BWANA na ayafurahie matendo yake.
32. Aitazama nchi, inatetemeka;Aigusa milima, inatoka moshi.
33. Nitamwimbia BWANA maadamu ninaishi;Nitamshangilia Mungu wangu nikiwa hai;
34. Kutafakari kwangu na kuwe kutamu kwake;Mimi nitamfurahia BWANA.