14. Huyameesha majani kwa makundi,Na maboga kwa matumizi ya mwanadamu;Ili atoe chakula katika nchi,
15. Na divai imfurahishe mtu moyo wake.Aung’aze uso wake kwa mafuta,Na mkate umburudishe mtu moyo wake.
16. Miti ya BWANA nayo imeshiba,Mierezi ya Lebanoni aliyoipanda.
17. Ndimo ndege wafanyamo vitundu vyao,Na korongo, misunobari ni nyumba yake.
18. Milima mirefu ndiko waliko mbuzi wa mwitu,Na magenge ni kimbilio la wibari.