1. Ee BWANA, usikie kuomba kwangu,Kilio changu kikufikie.
2. Usinifiche uso wako siku ya shida yangu,Unitegee sikio lako, siku niitapo unijibu upesi.
3. Maana siku zangu zinatoweka kama moshi,Na mifupa yangu inateketea kama kinga.
4. Moyo wangu umepigwa kama majani na kukauka,Naam, ninasahau kula chakula changu.
5. Kwa ajili ya sauti ya kuugua kwanguMifupa yangu imegandamana na nyama yangu.
6. Nimekuwa kama mwari nyuni wa jangwani,Na kufanana na bundi wa mahameni.
7. Nakesha, tena nimekuwa kama shomoroAliye peke yake juu ya nyumba.
8. Adui zangu wananilaumu mchana kutwa;Wanaonichukia kana kwamba wana wazimuHuapa kwa kunitaja mimi.