1. Ee BWANA, kwa nini wasimama mbali?Kwani kujificha nyakati za shida?
2. Kwa kiburi chake asiye haki mnyonge anafuatiwa kwa ukali;Na wanaswe kwa hila zizo hizo walizoziwaza.
3. Maana mdhalimu hujisifia tamaa ya nafsi yake,Na mwenye choyo humkana BWANA na kumdharau.
4. Mdhalimu kwa kiburi cha uso wakeAsema, Hatapatiliza.Jumla ya mawazo yake ni, Hakuna Mungu;
5. Njia zake ni thabiti kila wakati.Hukumu zako ziko juu asizione,Adui zake wote awafyonya.
6. Asema moyoni mwake, Sitaondoshwa,Kizazi baada ya kizazi sitakuwamo taabuni.
7. Kinywa chake kimejaa laana,Na hila na dhuluma.Chini ya ulimi wake kuna madhara na uovu,
8. Hukaa katika maoteo ya vijiji.Mahali pa siri humwua asiye na hatia,Macho yake humvizia mtu duni.