8. bali shikamaneni na BWANA, Mungu wenu, kama mlivyotenda hata hivi leo.
9. Maana BWANA amefukuza mbele yenu mataifa walio hodari, kisha wenye nguvu, lakini kwenu ninyi hapana mtu aliyesimama mbele yenu hata leo.
10. Mtu mmoja miongoni mwenu atafukuza watu elfu; maana BWANA, Mungu wenu, ndiye anayewapigania, kama alivyowaambia.
11. Jihadharini nafsi zenu, basi, ili mmpende BWANA, Mungu wenu.