38. na Ironi, na Migdal-eli, na Horemu, na Bethanathi, na Bethshemeshi; miji kumi na kenda, pamoja na vijiji vyake.
39. Huu ndio urithi wa kabila ya wana wa Naftali kwa kuandama jamaa zao; miji hiyo pamoja na vijiji vyake.
40. Kisha kura ya saba ilitokea kwa ajili ya kabila ya wana wa Dani kwa kuandama jamaa zao.
41. Na mpaka wa urithi wao ulikuwa ni Sora, na Eshtaoli, na Irishemeshi;
42. na Shaalabini, na Aiyaloni, na Ithla;
43. na Eloni, na Timna, na Ekroni;
44. na Elteka, na Gibethoni, na Baalathi;