Yos. 19:14-22 Swahili Union Version (SUV)

14. kisha mpaka uliizunguka nchi hiyo kwa upande wa kaskazini hata Hanathoni; kisha matokeo yake yalikuwa katika bonde la Iftaeli;

15. na Katathi, na Nahalali, na Shimroni, na Idala, na Bethlehemu; miji kumi na miwili, pamoja na vijiji vyake.

16. Huu ndio urithi wa wana wa Zabuloni kwa kuandama jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake.

17. Kisha kura ya nne ilitokea kwa ajili ya Isakari, maana, ni kwa ajili ya wana wa Isakari kwa kuandama jamaa zao.

18. Na mpaka wao ulifikilia Yezreeli, na Kesulothi, na Shunemu;

19. na Hafaraimu, na Shioni, na Anaharathi;

20. na Rabithu, na Kishioni, na Ebesi;

21. na Remethi, na Enganimu, na Enhada, na Bethpasesi;

22. na mpaka ukafikilia hata Tabori, na Shahasuma na Bethshemeshi; na matokeo ya mpaka wao yalikuwa katika mto wa Yordani; miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.

Yos. 19