15. Na upande wa kusini ulikuwa ukitoka upande wa mwisho wa Kiriath-yearimu, na mpaka ukatokea upande wa magharibi, ukaendelea hata chemchemi ya maji, pale Neftoa;
16. kisha mpaka ulitelemka hata mwisho wa mlima ulio pale mkabala wa bonde la mwana wa Hinomu, lililo pale katika bonde la Warefai, upande wa kaskazini; nao ukatelemkia mpaka bonde la Hinomu, hata ubavuni mwa Myebusi upande wa kusini, kisha ukatelemka hata Enrogeli,
17. kisha ulipigwa upande wa kaskazini, nao ukatokea hapo Enshemeshi, ukatokea hata kufikilia Gelilothi, ambao ni mkabala wa makweleo ya Adumimu; kisha ulitelemka hata jiwe la Bohani mwana wa Reubeni;
18. kisha ukaendelea mbele ubavuni kuikabili Araba, upande wa kuelekea kaskazini, nao ukatelemka hata hiyo Araba;
19. kisha mpaka ukaendelea mbele ubavuni mwa Beth-hogla upande wa kaskazini; na matokeo ya mpaka yalikuwa katika ile hori ya kaskazini ya Bahari ya Chumvi, mwisho wa kusini wa mto wa Yordani; huo ndio mpaka wa upande wa kusini.
20. Na mto wa Yordani ulikuwa ndio mpaka wake upande wa mashariki. Huo ndio urithi wa wana wa Benyamini, kwa kuandama mipaka yake kwa kuuzunguka kote kote, sawasawa na jamaa zao.
21. Basi miji ya kabila ya wana wa Benyamini kwa kuandama jamaa zao ilikuwa ni Yeriko, na Beth-hogla, na Emek-kesisi,
22. na Bethiaraba, na Semaraimu, na Betheli;
23. na Avimu, na Para, na Ofra;