55. Maoni, na Karmeli, na Zifu, na Yuta;
56. na Yezreeli, na Yokdeamu, na Zanoa;
57. na Kaini, na Gibea, na Timna; miji kumi, pamoja na vijiji vyake.
58. Halhuli, na Bethsuri, na Gedori;
59. na Maarathi, na Bethanothi, Eltekoni; miji sita, pamoja na vijiji vyake.
60. Kiriath-baali (ndio Kiriath-yearimu), na Raba; miji miwili, pamoja vijiji vyake.
61. Huko nyikani, Betharaba, na Midini, na Sekaka;
62. na Nibshani, na huo Mji wa Chumvi, na Engedi; miji sita, pamoja na vijiji vyake.
63. Tena katika habari ya Wayebusi, hao wenye kukaa Yerusalemu, wana wa Yuda hawakuweza kuwatoa; lakini hao Wayebusi walikaa pamoja na wana wa Yuda huko Yerusalemu hata hivi leo.