46. kutoka huko Ekroni mpaka baharini, yote iliyokuwa upande wa Ashdodi, pamoja na vijiji vyake.
47. Ashdodi, na miji yake na vijiji vyake; na Gaza, na miji yake na vijiji vyake; mpaka kijito cha Misri, na bahari kubwa, na mpaka wake.
48. Na katika nchi ya vilima, Shamiri, na Yatiri, na Soko;
49. na Dana, na Kiriath-sana (ambao ni Debiri);
50. na Anabu, na Eshtemoa, na Animu;
51. na Gosheni, na Holoni, na Gilo; miji kumi na mmoja, pamoja na vijiji vyake.
52. Arabu, na Duma, na Eshani;
53. na Yanumu, na Beth-tapua, na Afeka;
54. na Humta, na Kiriath-arba (ndio Hebroni), na Siori; miji kenda, pamoja na vijiji vyake.
55. Maoni, na Karmeli, na Zifu, na Yuta;
56. na Yezreeli, na Yokdeamu, na Zanoa;
57. na Kaini, na Gibea, na Timna; miji kumi, pamoja na vijiji vyake.
58. Halhuli, na Bethsuri, na Gedori;
59. na Maarathi, na Bethanothi, Eltekoni; miji sita, pamoja na vijiji vyake.
60. Kiriath-baali (ndio Kiriath-yearimu), na Raba; miji miwili, pamoja vijiji vyake.
61. Huko nyikani, Betharaba, na Midini, na Sekaka;
62. na Nibshani, na huo Mji wa Chumvi, na Engedi; miji sita, pamoja na vijiji vyake.