21. Miji ya mwisho ya kabila ya wana wa Yuda upande wa kuelekea mpaka wa Edomu katika nchi ya Negebu ilikuwa ni Kabseeli, na Ederi, na Yaguri;
22. na Kina, na Dimona, na Adada;
23. na Kedeshi, na Hazori, na Ithnani;
24. na Zifu, na Telemu, na Bealothi;
25. na Hazor-hadata, na Kerioth-hezroni (ndio Hazori);
26. na Amamu, na Shema, na Molada;
27. na Hasar-gada, na Heshmoni, na Bethpeleti;
28. na Hasarshuali, na Beer-sheba, na Biziothia;
29. na Baala, na Iyimu, na Esemu;
30. na Eltoladi, na Kesili, na Horma;
31. na Siklagi, na Madmana, na Sansana;
32. na Lebaothi, na Shilhimu, na Aini, na Rimoni; miji hiyo yote ni miji ishirini na kenda, pamoja na vijiji vyake.
33. Katika nchi ya Shefela, Eshtaoli, na Sora, na Ashna,
34. na Zanoa, na Enganimu, na Tapua, na Enamu;