13. Kisha alimpa huyo Kalebu mwana wa Yefune sehemu kati ya wana wa Yuda, kama BWANA alivyomwamuru Yoshua, maana ni Kiriath-arba, ni huyo Arba aliyekuwa babaye Anaki (huo ndio Hebroni).
14. Huyo Kalebu aliwafukuza watoke hapo hao wana watatu wa Anaki, nao ni Sheshai, na Ahimani, na Talmai, wana wa Anaki.
15. Kisha akakwea kutoka huko ili kuwaendea wenyeji wa Debiri; jina la Debiri hapo kwanza lilikuwa Kiriath-seferi.
16. Kalebu akasema, Yeye atakayeupiga Kiriath-seferi na kuutwaa, mimi nitampa Aksa binti yangu awe mkewe.
17. Naye Othnieli mwana wa Kenazi, nduguye Kalebu, aliutwaa; basi akampa Aksa binti yake awe mkewe.
18. Kisha ikawa, hapo huyo mwanamke alipokwenda kwa mumewe, akamtaka aombe shamba kwa baba yake; akashuka katika punda wake; Kalebu akamwuliza, Wataka nini?
19. Huyo mwanamke akasema, Nipe baraka; kwa kuwa umeniweka katika nchi ya kusini, unipe na chemchemi za maji pia. Ndipo akampa chemchemi za maji ya juu, na chemchemi za maji ya chini.
20. Huu ndio urithi wa kabila ya wana wa Yuda sawasawa na jamaa zao.
21. Miji ya mwisho ya kabila ya wana wa Yuda upande wa kuelekea mpaka wa Edomu katika nchi ya Negebu ilikuwa ni Kabseeli, na Ederi, na Yaguri;
22. na Kina, na Dimona, na Adada;
23. na Kedeshi, na Hazori, na Ithnani;
24. na Zifu, na Telemu, na Bealothi;
25. na Hazor-hadata, na Kerioth-hezroni (ndio Hazori);
26. na Amamu, na Shema, na Molada;
27. na Hasar-gada, na Heshmoni, na Bethpeleti;
28. na Hasarshuali, na Beer-sheba, na Biziothia;