Lakini hakuwapa watu wa kabila ya Lawi urithi uwao wote; maana sadaka za BWANA, Mungu wa Israeli, zisongezwazo kwa njia ya moto ndizo urithi wake huyo, kama alivyomwambia.