Yos. 12:7-22 Swahili Union Version (SUV)

7. Hawa ni wafalme wa hiyo nchi ambao Yoshua na wana wa Israeli waliwapiga ng’ambo ya pili ya Yordani upande wa magharibi, kutoka Baal-gadi katika bonde la Lebanoni mpaka kilima cha Halaki, kilichoelekea Seiri; Yoshua naye akawapa kabila za Israeli iwe milki yao sawasawa na magawanyo yao;

8. katika nchi ya vilima, na katika Shefela, na katika nchi ya Araba, na katika matelemko, na katika bara, na katika Negebu; nchi ya Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi;

9. mfalme wa Yeriko, mmoja; mfalme wa Ai, ulio karibu na Betheli, mmoja;

10. mfalme wa Yerusalemu, mmoja; mfalme wa Hebroni, mmoja;

11. mfalme wa Yarmuthi, mmoja; na mfalme wa Lakishi, mmoja;

12. mfalme wa Egloni, mmoja; na mfalme wa Gezeri, mmoja;

13. mfalme wa Debiri, mmoja; na mfalme wa Gederi, mmoja;

14. mfalme wa Horma, mmoja; na mfalme wa Aradi, mmoja;

15. mfalme wa Libna, mmoja; na mfalme wa Adulamu, mmoja;

16. mfalme wa Makeda, mmoja; na mfalme wa Betheli, mmoja;

17. mfalme wa Tapua, mmoja; na mfalme wa Heferi, mmoja;

18. mfalme wa Afeka, mmoja; na mfalme wa Lasharoni, mmoja;

19. mfalme wa Madoni, mmoja; na mfalme wa Hazori, mmoja;

20. mfalme wa Shimron-meroni, mmoja; na mfalme wa Akshafu, mmoja;

21. mfalme wa Taanaki, mmoja; na mfalme wa Megido, mmoja;

22. na mfalme wa Kedeshi, mmoja; mfalme wa Yokneamu wa Karmeli, mmoja;

Yos. 12