7. Hawa ni wafalme wa hiyo nchi ambao Yoshua na wana wa Israeli waliwapiga ng’ambo ya pili ya Yordani upande wa magharibi, kutoka Baal-gadi katika bonde la Lebanoni mpaka kilima cha Halaki, kilichoelekea Seiri; Yoshua naye akawapa kabila za Israeli iwe milki yao sawasawa na magawanyo yao;
8. katika nchi ya vilima, na katika Shefela, na katika nchi ya Araba, na katika matelemko, na katika bara, na katika Negebu; nchi ya Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi;
9. mfalme wa Yeriko, mmoja; mfalme wa Ai, ulio karibu na Betheli, mmoja;
10. mfalme wa Yerusalemu, mmoja; mfalme wa Hebroni, mmoja;
11. mfalme wa Yarmuthi, mmoja; na mfalme wa Lakishi, mmoja;
12. mfalme wa Egloni, mmoja; na mfalme wa Gezeri, mmoja;
13. mfalme wa Debiri, mmoja; na mfalme wa Gederi, mmoja;
14. mfalme wa Horma, mmoja; na mfalme wa Aradi, mmoja;
15. mfalme wa Libna, mmoja; na mfalme wa Adulamu, mmoja;
16. mfalme wa Makeda, mmoja; na mfalme wa Betheli, mmoja;
17. mfalme wa Tapua, mmoja; na mfalme wa Heferi, mmoja;
18. mfalme wa Afeka, mmoja; na mfalme wa Lasharoni, mmoja;