Yos. 12:4-11 Swahili Union Version (SUV)

4. tena mpaka wa Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa wa hayo mabaki ya hao Warefai, aliyekaa Ashtarothi na Edrei,

5. naye alitawala katika mlima wa Hermoni, na katika Saleka, na katika Bashani yote, hata mpaka wa Wageshuri, na Wamaaka, na nusu ya Gileadi, mpaka wa huyo Sihoni mfalme wa Heshboni.

6. Musa mtumishi wa BWANA na wana wa Israeli wakawapiga; naye Musa mtumishi wa BWANA akawapa Wareubeni, na Wagadi, na nusu ya kabila ya Manase iwe urithi wao.

7. Hawa ni wafalme wa hiyo nchi ambao Yoshua na wana wa Israeli waliwapiga ng’ambo ya pili ya Yordani upande wa magharibi, kutoka Baal-gadi katika bonde la Lebanoni mpaka kilima cha Halaki, kilichoelekea Seiri; Yoshua naye akawapa kabila za Israeli iwe milki yao sawasawa na magawanyo yao;

8. katika nchi ya vilima, na katika Shefela, na katika nchi ya Araba, na katika matelemko, na katika bara, na katika Negebu; nchi ya Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi;

9. mfalme wa Yeriko, mmoja; mfalme wa Ai, ulio karibu na Betheli, mmoja;

10. mfalme wa Yerusalemu, mmoja; mfalme wa Hebroni, mmoja;

11. mfalme wa Yarmuthi, mmoja; na mfalme wa Lakishi, mmoja;

Yos. 12