3. na nchi ya Araba mpaka bahari ya Kinerethi, kuelekea mashariki, tena mpaka bahari ya Ataba, mpaka Bahari ya Chumvi, kwendea mashariki, njia ya kwendea Beth-yeshimothi; tena upande wa kusini, chini ya matelemko ya Pisga;
4. tena mpaka wa Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa wa hayo mabaki ya hao Warefai, aliyekaa Ashtarothi na Edrei,
5. naye alitawala katika mlima wa Hermoni, na katika Saleka, na katika Bashani yote, hata mpaka wa Wageshuri, na Wamaaka, na nusu ya Gileadi, mpaka wa huyo Sihoni mfalme wa Heshboni.
6. Musa mtumishi wa BWANA na wana wa Israeli wakawapiga; naye Musa mtumishi wa BWANA akawapa Wareubeni, na Wagadi, na nusu ya kabila ya Manase iwe urithi wao.