Yn. 8:35-39 Swahili Union Version (SUV)

35. Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote.

36. Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.

37. Najua ya kuwa ninyi ni uzao wa Ibrahimu lakini mnatafuta kuniua kwa sababu neno langu halimo ndani yenu.

38. Niliyoyaona kwa Baba ndiyo niyanenayo; nanyi vivyo hivyo mliyoyasikia kwa baba yenu ndiyo myatendayo.

39. Wakajibu, wakamwambia, Baba yetu ndiye Ibrahimu! Yesu akawaambia, Kama mngekuwa watoto wa Ibrahimu, mngezitenda kazi zake Ibrahimu.

Yn. 8