31. Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli;
32. tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
33. Wakamjibu, Sisi tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wasemaje, Mtawekwa huru?
34. Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.
35. Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote.
36. Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.