38. Wala neno lake hamnalo likikaa ndani yenu, kwa kuwa ninyi hammwamini yule aliyetumwa na yeye.
39. Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia.
40. Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima.
41. Mimi siupokei utukufu kwa wanadamu.
42. Walakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu.