39. Na katika mji ule Wasamaria wengi walimwamini kwa sababu ya neno la yule mwanamke, aliyeshuhudia kwamba, Aliniambia mambo yote niliyoyatenda.
40. Basi wale Wasamaria walipomwendea, walimsihi akae kwao; naye akakaa huko siku mbili.
41. Watu wengi zaidi wakaamini kwa sababu ya neno lake.
42. Wakamwambia yule mwanamke, Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako tu; maana sisi tumesikia wenyewe, tena twajua ya kuwa hakika huyu ndiye Mwokozi wa ulimwengu.
43. Na baada ya siku mbili hizo akaondoka huko, akaenda Galilaya.