Yn. 4:38-43 Swahili Union Version (SUV)

38. Mimi naliwatuma myavune yale msiyoyataabikia; wengine walitaabika, nanyi mmeingia katika taabu yao.

39. Na katika mji ule Wasamaria wengi walimwamini kwa sababu ya neno la yule mwanamke, aliyeshuhudia kwamba, Aliniambia mambo yote niliyoyatenda.

40. Basi wale Wasamaria walipomwendea, walimsihi akae kwao; naye akakaa huko siku mbili.

41. Watu wengi zaidi wakaamini kwa sababu ya neno lake.

42. Wakamwambia yule mwanamke, Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako tu; maana sisi tumesikia wenyewe, tena twajua ya kuwa hakika huyu ndiye Mwokozi wa ulimwengu.

43. Na baada ya siku mbili hizo akaondoka huko, akaenda Galilaya.

Yn. 4