1. Kwa hiyo Bwana, alipofahamu ya kuwa Mafarisayo wamesikia ya kwamba, Yesu anafanya wanafunzi wengi kuliko Yohana, na kuwabatiza,
2. (lakini Yesu mwenyewe hakubatiza, bali wanafunzi wake,)
3. aliacha Uyahudi, akaenda zake tena mpaka Galilaya.
4. Naye alikuwa hana budi kupita katikati ya Samaria.
5. Basi akafika kunako mji wa Samaria, uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa Yusufu mwanawe.