6. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
7. Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.
8. Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.
9. Nikodemo akajibu, akamwambia, Yawezaje kuwa mambo haya?
10. Yesu akajibu, akamwambia, Je! Wewe u mwalimu wa Israeli, na mambo haya huyafahamu?
11. Amin, amin, nakuambia kwamba, Lile tulijualo twalinena, na lile tuliloliona twalishuhudia; wala ushuhuda wetu hamwukubali.
12. Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, wala hamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mambo ya mbinguni?