Yn. 2:21-25 Swahili Union Version (SUV)

21. Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake.

22. Basi alipofufuka katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa alisema hivi, wakaliamini lile andiko na lile neno alilolinena Yesu.

23. Hata alipokuwapo Yerusalemu kwenye sikukuu wakati wa Pasaka, watu wengi waliamini jina lake, walipoziona ishara zake alizozifanya.

24. Lakini Yesu hakujiaminisha kwao; kwa kuwa yeye aliwajua wote;

25. na kwa sababu hakuwa na haja ya mtu kushuhudia habari za mwanadamu; kwa maana yeye mwenyewe alijua yaliyomo ndani ya mwanadamu.

Yn. 2