15. Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu.
16. Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.
17. Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.
18. Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni.
19. Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.
20. Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.
21. Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.