Yn. 15:12-15 Swahili Union Version (SUV)

12. Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi.

13. Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.

14. Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo.

15. Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.

Yn. 15