21. Naye alipokwisha kusema hayo, Yesu alifadhaika rohoni, akashuhudia akisema, Amin, amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti.
22. Wanafunzi wakatazamana, huku wakiona shaka ni nani amtajaye.
23. Na palikuwapo mmoja wa wanafunzi wake, ameegama kifuani pa Yesu, ambaye Yesu alimpenda.
24. Basi Simoni Petro akampungia mkono, akamwambia, Uliza, ni nani amtajaye?
25. Basi yeye, hali akimwelekea Yesu kifua chake, akamwambia, Bwana, ni nani?
26. Basi Yesu akajibu, Ndiye mtu yule nitakayemtowelea tonge na kumpa. Akatowelea tonge, akalitwaa akampa Yuda, mwana wa Simoni Iskariote.
27. Na baada ya hilo tonge Shetani alimwingia. Basi Yesu akamwambia, Uyatendayo yatende upesi.
28. Wala hakuna mtu katika wale walioketi chakulani aliyeijua sababu ya kumwambia hivyo.