4. Basi Yuda Iskariote, mmojawapo wa wanafunzi wake, ambaye ndiye atakaye kumsaliti, akasema,
5. Mbona marhamu hii haikuuzwa kwa dinari mia tatu, wakapewa maskini?
6. Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini; bali kwa kuwa ni mwivi, naye ndiye aliyeshika mfuko, akavichukua vilivyotiwa humo.
7. Basi Yesu alisema, Mwache aiweke kwa siku ya maziko yangu.
8. Kwa maana maskini mnao sikuzote pamoja nanyi; bali mimi hamnami sikuzote.
9. Basi watu wengi katika Wayahudi walipata kujua ya kuwa yeye yuko huko, nao wakaja, si kwa ajili yake Yesu tu, ila wamwone na Lazaro, ambaye Yesu alimfufua katika wafu.
10. Nao wakuu wa makuhani wakafanya shauri la kumwua Lazaro naye;
11. maana kwa ajili yake wengi katika Wayahudi walijitenga, wakamwamini Yesu.
12. Nayo siku ya pili yake watu wengi walioijia sikukuu walisikia ya kwamba Yesu anakuja Yerusalemu;