Yn. 11:1-10 Swahili Union Version (SUV)

1. Basi mtu mmoja alikuwa hawezi, Lazaro wa Bethania, mwenyeji wa mji wa Mariamu na Martha, dada yake.

2. Ndiye Mariamu yule aliyempaka Bwana marhamu, akamfuta miguu kwa nywele zake, ambaye Lazaro nduguye alikuwa hawezi.

3. Basi wale maumbu wakatuma ujumbe kwake wakisema, Bwana, yeye umpendaye hawezi.

4. Naye Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo.

5. Naye Yesu alimpenda Martha na umbu lake na Lazaro.

6. Basi aliposikia ya kwamba hawezi, alikaa bado siku mbili pale pale alipokuwapo.

7. Kisha, baada ya hayo, akawaambia wanafunzi wake, Twendeni Uyahudi tena.

8. Wale wanafunzi wakamwambia, Rabi, juzijuzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga kwa mawe, nawe unakwenda huko tena?

9. Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.

10. Bali akienda usiku hujikwaa; kwa sababu nuru haimo ndani yake.

Yn. 11