Yn. 10:5-9 Swahili Union Version (SUV)

5. Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni.

6. Mithali hiyo Yesu aliwaambia, lakini wao hawakuelewa na mambo hayo aliyowaambia.

7. Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo.

8. Wote walionitangulia ni wevi na wanyang’anyi; lakini kondoo hawakuwasikia.

9. Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.

Yn. 10