Yer. 7:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa BWANA, kusema,

2. Simama langoni pa nyumba ya BWANA, ukatangaze hapo neno hili, ukisema, Sikilizeni neno la BWANA, ninyi nyote wa Yuda, mnaoingia katika malango haya ili kumwabudu BWANA.

3. BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tengenezeni njia zenu, na matendo yenu, nami nitawakalisha ninyi mahali hapa.

Yer. 7