Yer. 52:2-9 Swahili Union Version (SUV)

2. Naye alitenda yaliyo mabaya machoni pa BWANA, sawasawa na yote aliyoyatenda Yehoyakimu.

3. Maana, kwa sababu ya hasira ya BWANA, mambo haya yalitokea katika Yerusalemu na katika Yuda, hata akawaondosha wasiwe mbele za uso wake, naye Sedekia akamwasi mfalme wa Babeli.

4. Ikawa, katika mwaka wa kenda wa kumiliki kwake, katika mwezi wa kumi, na siku ya kumi ya mwezi huo, Nebukadreza, mfalme wa Babeli, akaja, yeye na jeshi lake lote, juu ya Yerusalemu, akapanga hema zake juu yake; nao wakajenga ngome juu yake pande zote.

5. Basi mji huo ulihusuriwa hata mwaka wa kumi na mmoja wa mfalme Sedekia.

6. Katika mwezi wa nne, siku ya kenda ya mwezi, njaa ilizidi sana ndani ya mji, hata hapakuwa na chakula kwa watu wa nchi.

7. Ukuta wa mji ukabomolewa, watu wote wa vita wakakimbia, wakatoka mjini usiku, kwa njia ya lango lililokuwa kati ya zile kuta mbili, karibu na bustani ya mfalme; (basi wale Wakaldayo walikuwa wameuzunguka mji pande zote;) wakaenda zao kwa njia ya Araba.

8. Lakini jeshi la Wakaldayo wakamfuatia mfalme, wakampata Sedekia katika nchi tambarare ya Yeriko, na jeshi lake lote walikuwa wametawanyika na kumwacha.

9. Nao wakamshika mfalme, wakamchukua kwa mfalme wa Babeli, aliyekuwa huko Ribla katika nchi ya Hamathi, naye akatoa hukumu juu yake.

Yer. 52