Na nguzo za shaba zilizokuwa katika nyumba ya BWANA, na matako ya bahari ya shaba iliyokuwa katika nyumba ya BWANA, Wakaldayo walivivunja vipande vipande, wakaichukua shaba yake yote mpaka Babeli.