7. Babeli umekuwa kikombe cha dhahabu mkononi mwa BWANA; kilicholevya dunia yote; mataifa wamekunywa mvinyo wake; kwa sababu hiyo mataifa wameingiwa na wazimu.
8. Babeli umeanguka na kuangamia ghafula; mpigieni yowe; twaeni zeri kwa maumivu yake; ili labda apate kuponywa.
9. Tungependa kuuponya Babeli,Lakini haukuponyeka;Mwacheni, nasi twendeni zetu,Kila mtu hata nchi yake mwenyewe;Maana hukumu yake inafika hata mbinguni,Nayo imeinuliwa kufikilia mawinguni.
10. BWANA ameitokeza haki yetu;Njoni, tutangaze katika SayuniHabari za kazi ya BWANA, Mungu wetu.